Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Bahram Einollahi alisema hayo jana na kuongeza kuwa ifikapo mwishoni mwa mwezi wa Kiirani wa Shahrivar sawa na tarehe 22 Septemba 2021, Iran itakuwa imeshapiga chanjo milioni 50 humu nchini.
Amesema, kwa juhudi za Rais Ebrahim Raisi na Makamu wa Kwanza wa Rais, Mohammad Mokhber, hivi sasa zaidi ya dozi milioni 38 za chanjo ya corona zimeshapigwa humu nchini.
Vile vile amesema, karibuni hivi watu wote wenye nia ya kusafiri nje ya Iran watatakiwa wawe wameshapiga chanjo kamili za corona na wale ambao hawajapata chanjo kamili watalazimika kuchukua vipimo vya UVIKO-19 kutoka nchi wanayotoka na wakati wanapofika hapa nchini.
Huku hayo yakiripotiwa, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani, WHO usiku wa kuamkia leo amelalamikia vikali dhulma na ubaguzi unaofanywa katika ugawaji wa chanjo za corona duniani akisema kuwa, hadi hivi sasa nchi za bara la Afrika zimepatiwa asilimia 2 tu ya chanjo zilizogaiwa duniani.
Dk Tedros Adhanom amesema kuwa, hali hiyo ni doa la aibu kwa dunia na litabakia hivyo milele. Amekiri kwamba nchi tajiri zimefunga njia za kufika chanjo za corona barani Afrika.
Maafisa wa ngazi za juu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) nao wamezitaka nchi tajiri ikiwemo Marekani kuruhusu kufikishwa chanjo za corona kwa nchi maskini badala ya kutumia chanjo hizo kujipiga wenyewe nchi tajiri kwa madai ya kutia nguvu chanjo kamili walizopigwa wananchi wa nchi hizo.
342/